Xi atoa salamu za mwaka mpya wa jadi kwa Wachina wote
2024-02-09 08:43:49| cri

Kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la Serikali, Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa Wachina wote kwenye tafrija iliyofanyika jana Alhamis kwenye Jumba la Mikutano ya Umma hapa mjini Beijing.

Rais Xi amesema Mwaka wa Sungura ambao unamalizika, umekuwa mwanzo wa utekelezaji kamili wa kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti katika nyanja zote, akibainisha kuwa China inakabiliwa na mazingira yenye utata ya kimataifa na kazi ngumu za mageuzi, maendeleo na kudumisha utulivu.

Rais Xi ameongeza kuwa China imeunganisha nguvu pamoja kuelekea China ya kisasa, huku ikizingatia mazingira ya ndani na ya kimataifa, kushinda taabu na changamoto nyingi, na kupiga hatua thabiti katika safari mpya ya kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya ujamaa kwa pande zote.