Serikali ya Iraq imesema, Iraq na Marekani zimerejesha duru mpya ya mazungumzo ili kujadili kuhusu kumaliza operesheni ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani nchini Iraq.
Msemaji wa jeshi la Iraq Bw. Yahya Rasoul ametoa taarifa akisema, kamati ya jeshi ya ngazi ya juu HMC imerejesha mikutano na upande wa muungano wa kimataifa, ili kutathmini hali ya jeshi, kiwango cha tishio linalosababishwa na kundi la IS pamoja na uwezo wa vikosi vya Iraq.
Bw. Rasoul amesema, juu ya msingi wa mikutano hiyo, itawekwa ratiba ya kupunguza kwa utaratibu kiasi cha washauri wa muungano wa kimataifa nchini Iraq, ikilenga kumaliza operesheni ya muungano huo kupambana na kundi la IS na mpito wa uhusiano wa pande mbili kati ya Iraq na nchi za muungano.