Watu watatu wafariki na wengine 18 kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi kusini mwa Tanzania
2024-02-12 09:21:09| CRI

Wanakijiji watatu wamefariki na wengine 18 kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi Ijumaa iliyopita wakati waliposhiriki kwenye mazishi katika mkoa wa Lindi, kusini mwa Tanzania.

Msimamizi wa kituo cha afya cha eneo la Mtama mkoani humo Abdallah Mputa amesema janga hilo lilitokea baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha radi ikiwapiga saa kumi alasiri kwa saa za huko. Hivi sasa watu waliojeruhiwa wanaendelea kupewa matibabu katika kituo hicho cha afya.