Israel inakabiliwa na shinikizo la kikanda na kimataifa kutokana na mpango wake wa kushambulia Rafah, mji wa kusini mwa ukanda ya Gaza.
Katika siku kadhaa zilizopita, nchi za kanda hiyo zimeionya Israel kuwa Rafah itakabiliwa na mgogoro wa kibinadamu kama kikosi cha Israel kitafanya shambulizi la ardhini katika mji huo ambao watu zaidi ya milioni 1.4 wa Palestina wanaishi wakiwemo watu milioni 1.3 waliokimbia sehemu za kaskazini.
Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu amesema, amelielekeza jeshi kujiandaa kuwahamisha raia wa kawaida kutoka Rafah mji wenye watu wengi kabla ya kupanua shambulizi dhidi ya kundi la Hamas.
Hoja hiyo imezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa nchi za kanda hiyo kwamba mpango huo utazidisha hali mbaya ya kibinadamu tangu mapigano kati ya Israel na Hamas yazuke Oktoba 7 mwaka jana.