Takriban wanajeshi watatu wa UAE wauawa katika shambulio nchini Somalia
2024-02-12 09:10:18| CRI

Takriban wanajeshi watatu wa Vikosi vya Wanajeshi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) waliuawa katika shambulio lililotokea Jumamosi jioni kwenye kambi ya kijeshi huko Mogadishu, nchini Somalia.

Ikithibitisha shambulio hilo jana Jumapili Wizara ya Ulinzi ya UAE imesema mashambulizi hayo ambayo yalilenga wanajeshi katika kambi ya kijeshi ya Jenerali Gordon pia yalipelekea kujeruhiwa kwa maafisa watatu wa Jeshi la Ulinzi la Bahrain na Jeshi la Kitaifa la Somalia (SNA).

Serikali ya Somalia haijatoa maelezo ya kina kuhusu shambulio lililohusika.

Vifo hivyo vilitokea baada ya askari kuruta wa jeshi la Somalia kufyatua bunduki yake akiwalenga wanajeshi waliokuwa ndani ya kituo cha kijeshi.Wanajeshi wa UAE walikuwa kwenye mafunzo ya Jeshi la Kitaifa la Somalia kama sehemu ya makubaliano ya nchi mbili kati ya UAE na Somalia.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amelaani tukio hilo na kutoa rambirambi zake kwa serikali na watu wa UAE kwa maafisa waliopoteza maisha huko Mogadishu.