Watoto wawili wa shule wafariki na wengine 20 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea nchini Cameroon
2024-02-12 09:23:57| cri

Watu wawili walikufa na wengine 20 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea siku ya Jumapili katika mji wa Nkambe uliopo kwenye eneo linaloongea Kingereza la Kaskazini-magharibi nchini Cameroon, ambapo wengi walioathirika ni watoto wa shule.

Kwa mujibu wa mashahidi na polisi wa eneo hilo, Mlipuko huo ulitokea wakati watoto wa shule wakishiriki katika shughuli za kuadhimisha Siku ya Vijana ya Kitaifa.

Vyanzo kutoka idara ya usalama katika eneo hilo waliiambia Xinhua kuwa, watumishi wa afya wamejitahidi sana kuwatibu watoto wengi ambao walikuwa na majeraha mabaya sana.

Vyanzo hivyo pia vimesema, idadi ya vifo inaweza kuongezeka, huku vikiongeza kuwa hali ni ya kutatanisha lakini askari wao jasiri wameimarisha ulinzi ili kuwasaka magaidi waliofanya kitendo hiki cha kuchukiza.