Jeshi la Sudan Kusini laahidi kuacha kuandikisha watoto jeshini
2024-02-13 09:51:39| CRI

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) Jumatatu lilisisitiza dhamira yake ya kukomesha kuandikisha watoto katika jeshi la taifa.

Akiongea huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya askari watoto, mkurugenzi wa ulinzi wa watoto katika SSPDF, Chaplain Khamis Edward, alisema imeonekana kuwa kuwatumia watoto katika migogoro ya kivita ni ukiukwaji mkubwa na ndiyo maana wanapinga kuajiri watoto wakati huohuo wakidhamiria kusaini mipango mingi ya kukomesha kabisa suala hili la kuajiri na kuwatumia watoto nchini Sudan Kusini.

Khamis alibainisha kuwa SSPDF ingewaondoa askari watoto tangu 2009 au 2012, lakini kutokana na ukosefu wa usalama unaojitokeza mara kwa mara nchini Sudan Kusini, ndiyo maana bado wanazungumzia kuhusu ukiukwaji wa haki za watoto nchini humo.