Mapigano nchini Sudan yasababisha watu zaidi ya laki 5.4 kuingia nchini Sudan Kusini
2024-02-13 09:07:54| CRI

Ofisi ya Uratibu ya Mambo ya Kibindamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) jana ilisema kuwa mapigano kati ya jeshi la Sudan (SAF) na vikosi vya msaada wa haraka (RSF) nchini Sudan yamesababisha watu laki 5.42 kukimbia na kwenda nchini Sudan Kusini tangu katikati ya Aprili mwaka jana, na kati yao asilimia 80 ni wananchi wa Sudan Kusini na asilimia 19 ni wa Sudan, ikionesha kuwa sasa bado kuna watu wengi wanaokimbia Sudan huku idadi ya Wasudan kati yao ikiongezeka.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mapigano hayo nchini Sudan yamesababisha watu zaidi ya elfu tisa kuuawa na wengine milioni sita kukimbia makazi yao ndani na nje ya nchi hiyo, huku watu milioni 25 wakihitaji msaada.