Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China amesema kuwa China inatilia maanani sana hali ya eneo la Rafah. Pia ameeleza kuwa inapinga na kulaani vitendo vya kudhuru raia na kukiuka sheria za kimataifa, ambapo inaitaka Israel isimamishe operesheni za kijeshi haraka iwezekanavyo.
Amesema hayo wakati akijibu maswali ya wanahabari waliotaka kujua China ina maoni gani kuhusu mashambulizi makubwa ya anga yaliyofanywa na jeshi la Israel katika eneo la Rafah kusini mwa Gaza ambayo yamesababisha vifo na majeruhi. Msemaji huyo pia amebainisha kuwa China inaitaka Israel ifanye kila juhudi kuepusha majeruhi ya raia wasio na hatia, na kuzuia maafa makubwa zaidi ya kibinadamu katika eneo la Rafah.