AU yaazimia kushirikiana na Somalia licha ya wanajeshi watano wa kigeni kuuawa nchini humo
2024-02-13 09:12:04| cri

Tume ya Mpito yaa Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) Jumatatu imelaani tukio la Jumamosi ambapo maafisa waandamizi watano wa kijeshi waliuawa, huku ikiahidi kushirikiana na nchi hiyo kupambana na ugaidi.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, Mohamed El-Amine Souef alithibitisha kuwa, maafisa wanne wa kijeshi kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na mmoja kutoka Bahrain, waliuawa kwa kupigwa risasi katika kambi ya kijeshi ya Jenerali Gordon, inayoendeshwa na UAE.

Kwa niaba ya ATMIS, Bw. Souef alilaani shambulizi dhidi ya wakufunzi wa kijeshi na askari wa Somalia kwenye kambi hiyo, ambao walikuwa wakifanya kazi ya kuendeleza juhudi za usalama nchini Somalia. ATMIS inaendeleza nia yake ya dhati ya kufanya kazi na watu na serikali ya Somalia, pamoja na washirika wa kimataifa katika mapambano dhidi ya ugaidi.