Tanzania yashuhudia ongezeko la wagonjwa wa kifafa miongoni mwa vijana
2024-02-13 09:50:55| CRI

Wakati Tanzania ikiadhimisha Siku ya Kifafa Duniani jana Jumatatu, daktari mshauri wa magonjwa ya mishipa ya fahamu kutoka Chama cha Kifafa Tanzania (TEA), Patience Njenje amesema vijana wenye umri wa miaka 15 na kuendelea wanaongoza kwa kuugua kifafa, hasa kinachosababishwa na ajali.

Daktari Njenje alibainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye wagonjwa wengi wa kifafa barani Afrika, ikiwa na wastani wa wagonjwa 37 kati ya 1,000 na kuongeza kuwa ajali nyingi zinazosababisha kifafa hicho ni za pikipiki, kwani pikipiki nyingi nchini Tanzania zinaendeshwa na vijana.Njenje amesema Afrika ina asilimia kubwa ya watu wanaoishi na kifafa ambapo kuna wagonjwa 20 hadi 58 kwa kila watu 1,000.

Siku ya Kifafa Duniani, inayoadhimishwa Jumatatu ya pili ya Februari kila mwaka ni fursa ya kuongeza ufahamu wa ugonjwa wa kifafa.