Mkuu anayeshughulikia misaada ya UM anaonya operesheni za kijeshi za Israel huko Rafah zinaweza kusababisha mauaji
2024-02-14 09:28:33| CRI

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu Martin Griffiths alionya Jumanne kwamba Operesheni za kijeshi za Rafah zinaweza kusababisha mauaji huko Gaza na kuweka operesheni dhaifu ya kibinadamu kwenye mlango wa kifo.

Katika taarifa yake iliyotolewa Geneva, alibainisha onyo lililotolewa na jamii ya kimataifa dhidi ya matokeo ya hatari ya uvamizi wa ardhini huko Rafah kusini mwa Gaza, akisema kuwa serikali ya Israel haipaswi kuendelea kupuuza wito huu. Alisisitiza kuwa watu wa Rafah na maeneo mengine ya Gaza ni wahanga wa shambulio ambalo ukali wake, ukatili na upeo wake hauna kifani.

Wakati huohuo televisheni ya al-Qahera imemnukuu afisa wa ngazi ya juu wa Misri akisema kuwa mazungumzo ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza unaokumbwa na vita, ambayo yanaendelea mjini Cairo nchini Misri, ni "chanya".

Mkutano wa usalama wa pande nne uliohudhuriwa na Misri, Marekani, Qatar na Israel ulianza Jumanne mjini Cairo kujadili uwezeshaji wa kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza na kubadilishana wafungwa.