Naibu waziri mkuu wa DRC asema jeshi la taifa na MONUSCO wanapambana na M23 kwa pamoja
2024-02-14 09:25:31| CRI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jean-Pierre Bemba amesema Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO kinashirikana na kikosi cha jeshi la taifa la DRC FARDC katika kupambana na kundi la waasi la M23 mashariki mwa nchi hiyo, licha ya kuendelea na mchakato wa kujiondoa kwake.

Bemba aliyasema hayo Jumanne mjini Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, ambako hali ya wasiwasi imeongezeka kutokana na mapigano makali kati ya jeshi la taifa la DRC na kundi la M23 katika mji wa Sake na maeneo ya karibu, takriban kilomita 23 ya kaskazini magharibi mwa Goma.

Ufafanuzi huo unalenga kusahihisha uvumi kwamba MONUSCO na M23 wanashirikiana pamoja.