Watanzania watoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa
2024-02-14 09:26:14| CRI

Mamia ya Watanzania jana walitoa heshima zao za mwisho kwa waziri mkuu wao wa zamani Bw. Edward Lowassa, aliyefariki Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mrefu akiwa na umri wa miaka 70.

Mwili wa Bw. Lowassa  uliagwa katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es Salaam huku mtu mmoja baada ya mwingine akitoa heshima za mwisho kwa Bw. Lowassa aliyefariki katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Siku ya Jumapili, waziri mkuu Bw. Majaliwa alitangaza kuwa Bw. Lowassa atazikwa kijijini kwao Ngarash wilayani Monduli mkoani Arusha Februari 17, ambapo rais Samia Suluhu Hassan atahudhuria mazishi yake.