IMF yapongeza kuimarika kwa uchumi wa Zimbabwe huku kukiwa na msukosuko wa sarafu
2024-02-15 09:29:04| cri

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lilisema Jumatano kuwa shughuli za kiuchumi nchini Zimbabwe zinaendelea kuonesha uthabiti katika kukabiliana na kuyumba kwa sarafu na mfumuko mkubwa wa bei.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa mwishoni mwa ziara ya wiki mbili ya wafanyakazi wake nchini Zimbabwe, IMF ilisema wakati ukuaji unatarajiwa kushuka hadi takriban asilimia 3.25 mwaka 2024 kutokana na uzalishaji wa kilimo kuathiriwa na ukame na bei ya chini ya bidhaa, utumaji fedha kutoka nje utaendelea kuwa na nguvu na kukabiliana na kupungua kwa uingiaji wa fedha za kigeni unaotarajiwa.

Uchumi wa Zimbabwe ulikua kwa asilimia 5.3 mwaka 2023 kutokana na kupanuka kwa kilimo na madini.

Hata hivyo, IMF ilibainisha kuwa kuyumba kwa fedha za nchi hiyo kumeongezeka zaidi katika miezi michache iliyopita, huku kiwango rasmi cha ubadilishaji kikishuka kwa takriban asilimia 95 tangu mwanzoni mwa Disemba 2023.