Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU ataka suluhu ya kisiasa ili kutatua mgogoro kati ya Israel na Palestina
2024-02-15 09:25:19| cri

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametaka kuwepo suluhu ya kisiasa ili kutatua mgogoro kati ya Israel na Palestina.

Bw. Faki ametoa wito huo wakati alipohutubia Kikao cha Kawaida cha 44 cha Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika, akisema umoja huo ulitaka kuwepo kwa suluhu ya kisiasa tangu mwanzoni kabisa mwa mgogoro huo, ambayo ingefikiwa katika msingi wa kulinda amani kati ya Israel na Palestina, kuheshimu sheria ya kimataifa na kuhakikisha usalama wa watu wa nchi hizo mbili na wale walioko katika kanda hiyo.

Akibainisha kuwa amani na usalama vinaweza kupatikana tu kwa haki na kutambua haki za kimsingi za pande husika, Faki amekaribisha uamuzi ulitolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) baada ya Afrika Kusini kufungua kesi dhidi ya Israel mwezi Desemba mwaka jana, na ICJ kuitaka Israel kuchukua hatua zote zinazowezekana kuzuia mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.