Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika waanza mkutano wa Baraza la Utendaji la AU
2024-02-15 09:28:32| cri

Kikao cha Kawaida cha 44 cha Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika (AU) kilianza Jumatano katika makao makuu ya AU huko Addis Ababa, nchini Ethiopia, kikitoa wito wa kuongeza juhudi ili kuhakikisha utulivu na elimu bora barani Afrika.

Mkutano huo wa siku mbili, unaojumuisha mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi wanachama wa AU, unafanyika chini ya kaulimbiu ya "Mwelimishe Mwafrika ili afae katika Karne ya 21: Kujenga mifumo thabiti ya elimu kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa mafunzo jumuishi, ya maisha, yenye ubora, na muhimu katika Afrika."

Akihutubia kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat alisisitiza haja ya kufanya juhudi za pamoja ili kuhakikisha amani na usalama wa bara, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, ufadhili endelevu wa AU pamoja na kuimarisha mfumo wa pande nyingi wa kimataifa.