Mtu mmoja afariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulizi kwenye maandamano ya Super Bowl nchini Marekani
2024-02-15 09:26:03| cri

Mkuu wa idara ya polisi ya Mji wa Kansas jimboni Missouri, Bibi Stacey Graves, alisema jumatano, mtu mmoja aliuawa na wengine kumi hadi 15 kujeruhiwa baada ya shambulizi la kufyatua risasi kuibuka kwenye maandamano ya ushindi wa Super Bowl ya Mji wa Kansas nchini Marekani.

Msemaji wa Polisi ya Kansas Bw. Jake Becchina alisema, polisi wamewashikilia watu wawili wenye silaha kwa uchunguzi zaidi.

Gavana wa Kansas Bibi Laura Kelly aliyehamishwa kwenye eneo la maandamano, aliandika kwenye mtandao wa X akimuhimiza kila mtu kufuata maagizo na taarifa zaidi kutoka kwa polisi.