Wang Yi kuhudhuria Mkutano wa Usalama wa Munich, na kufanya ziara nchini Uhispania na Ufaransa
2024-02-15 15:50:50| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema kufuatia mwaliko kutoka kwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Usalama wa Munich Christoph Heusgen, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania José Manuel Albares Bueno, na Mshauri wa Mambo ya Nje wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Bonne, Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi atahudhuria Mkutano wa 60 wa Usalama wa Munich kuanzia Februari 16 hadi 21 ambapo atatoa hotuba kuhusu China na kufafanua msimamo wa China kuhusu masuala makubwa ya kimataifa kwa kuzingatia mada ya mkutano huo. Pia atafanya ziara nchini Uhispania na Ufaransa, na kufanya Mazungumzo ya Kimkakati kati ya China na Ufaransa nchini Ufaransa.