Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia atoa wito kwa AU kushiriki kikamilifu katika G20
2024-02-16 09:21:32| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Taye Atske Selassie ametoa wito kwa Umoja wa Afrika (AU) kushiriki kikamilifu katika Kundi la nchi 20 (G20) ili kusaidia sauti za Afrika kusikika katika nyanja ya kimataifa.

Bw. Selassie alitoa wito huo Jumatano wakati wa ufunguzi wa Kikao cha 44 cha Kawaida cha Baraza la Utendaji la AU huko Addis Ababa, Ethiopia. Aliongeza kuwa ushiriki kamili wa AU katika G20 utaipatia Afrika jukwaa la kipekee la kuchangia katika usimamizi wa kimataifa na kufanya maamuzi. Hivyo amesisitiza kuwa ni lazima, kuhakikisha kwamba sauti za Afrika zinasikika na kwamba ushiriki wake uwe na maana.

AU ilipewa hadhi kamili ya kuwa mwanachama katika mkutano wa kilele wa G20 mjini New Delhi, India, Septemba 2023. Kabla ya AU kujiunga na kundi hilo, Afrika Kusini ilikuwa nchi pekee ya Afrika kuwa na kiti katika G20.