Chuo Kikuu cha Kenyatta chafanya maonyesho ya dragoni wa China ili kukuza mawasiliano ya kitamaduni
2024-02-16 09:25:32| CRI

Maonyesho ya kisanii yanayolenga kuonyesha sifa tofauti za dragoni wa China yamefanyika Alhamisi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya.

Hafla hiyo ya iliyofanyika kwa siku nzima, na kupewa jina la Maonyesho ya Ubunifu wa Dragoni, iliangazia kazi za sanaa zaidi ya 40 na kuandaliwa na Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Ufundi ya Shandong. Walimu na wafanyakazi, wanafunzi na umma wameshiriki kwenye maonyesho ya michoro ya ukutani na picha za michoro, ambayo iliwasilisha sifa mbalimbali za dragoni wa China.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, Zhou Xiaodong alisema maonyesho hayo yaliyofanyika wakati sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China inaendelea, yatasaidia kuonesha utajiri wa utamaduni wa China kwa watu wa Kenya. Amesema mwaka 2024 ni mwaka wa dragoni, au Loong kwa kichina, unaashiria bahati, ustawi na nguvu, akibainisha kuwa maonyesho hayo yamefanyika wakati muafaka ili kusaidia kuongeza uelewa wa tamaduni mbalimbali.