Nchi wanachama wa EAC zathibitisha tena azama yao ya kuendeleza vyanzo vya nishati mbadala
2024-02-16 09:22:57| CRI

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumatano zilisisitiza azma yao ya kuimarisha ufanisi wa nishati na kutumia nishati ya upepo, jua na jotoardhi kama vyanzo vya nishati endelevu vya kanda hiyo.

Taarifa iliyotolewa Jumatano na Makao Makuu ya EAC mwishoni mwa kikao cha Mawaziri cha Baraza la 16 la Kisekta la Nishati kilichofanyika Arusha, Tanzania, ilisema nchi wanachama wa EAC zimeazimia kuanza mipango mbalimbali inayolenga kutumia uwezo wa nishati mbadala na uhifadhi wa nishati.

Mipango hiyo ni pamoja na mapitio ya sheria za kitaifa za nishati mbadala, utekelezaji wa kanuni za usimamizi wa nishati, mikakati na viwango vya kitaifa vya ufanisi wa nishati na nishati mbadala, na kukuza ufanisi na uhifadhi wa nishati.

Nchi wanachama wa EAC ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda, Tanzania na Somalia.