Watu sita wauawa na wengine 17 nchini Russia kujeruhiwa kwenye shambulio la roketi la Ukraine
2024-02-16 09:24:27| CRI

Wizara ya Afya ya Russia imesema watu sita wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa katika shambulio la roketi la Ukraine huko Belgorod nchini humo.

Wizara hiyo imesema shambulio hilo lililenga kituo cha maduka cha Belgorod, na kusababisha vifo na majeruhi, akiwemo mtoto mmoja kufariki dunia na watoto wanne kati yao kujeruhiwa.

Shirika la habari la Russia RIA limesema katika ripoti yake ya awali kuwa kituo cha maduka ambacho kina maduka ya mboga na dawa, kiliharibiwa vibaya kwenye shambulio hilo la roketi lililofanywa na wanajeshi wa Ukraine.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Russia, walinzi wa anga wa nchi hiyo walirusha chini roketi 14 za RM-70 Vampire MLRS katika eneo la Belgorod.