China kuendelea na jukumu la kiujenzi katika kurejesha amani nchini Ukraine
2024-02-19 10:20:50| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kuwa China itaendelea kubeba jukumu la kiujenzi katika kumaliza mapema mzozo na kurejesha amani nchini Ukraine, na haitakata tamaa maadamu kuna mwanga wa matumaini.

Bw. Wang alisema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba kando ya Mkutano wa Usalama wa Munich unaoendelea. Wang amefafanua msimamo wa China kuhusu suala la Ukraine, akisisitiza kwamba China inazingatia utatuzi wa kisiasa wa masuala nyeti na kuhimiza mazungumzo ya amani, pia haichochei zaidi migogoro, hainufaiki na hali hiyo, wala kuuza silaha hatari kwa maeneo na pande zinazohusika katika migogoro.

Kwa upande wake, Kuleba amesema kuwa Ukraine inatumai kuwa China itaendelea na jukumu la kipekee la kiujenzi katika kuhimiza amani, na inapenda kuimarisha mawasiliano na mwakilishi maalum wa serikali ya China kuhusu masuala ya Eurasia.