Mkutano wa kilele wa AU wataka kuwepo mshikamano wa kimataifa kwa Palestina
2024-02-19 10:31:30| CRI

Viongozi wa Afrika Jumamosi walihimiza "kukomeshwa mara moja" kwa mzozo wa Palestina na Israel, wakitoa wito wa kuwepo mshikamano wa kimataifa kwa Palestina wakati wa mkutano wa 37 wa Umoja wa Afrika (AU).

Akiongea kwenye ufunguzi wa Kikao cha 37 cha Kawaida cha Baraza la AU la Wakuu wa Nchi na Serikali, mwenyekiti wa AU wa mwaka 2024 na rais wa Mauritania, Mohamed Ould Cheikh Ghazouani, alisema hali ya sasa ya Gaza ni kielelezo dhahiri cha umuhimu wa mageuzi ndani ya mfumo wa kimataifa ulio na dhuluma kubwa na viwango vinavyotofautiana. Aliwaambia viongozi wa Afrika kuwa ni muhimu kutambua haki ya asili ya Wapalestina ya kuanzisha taifa lao huru, na Jerusalem Mashariki ukiwa mji mkuu wake, kwa kuzingatia maazimio muhimu ya uhalali wa kimataifa.

Pia alielezea wasiwasi wake juu ya kusitasita kwa jumuiya ya kimataifa kutoa ushawishi unaohitajika kwa ajili ya usitishaji mapigano mara moja, kutoa misaada, na kuanzishwa kwa suluhu ya kina na ya kudumu.

Naye Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Moussa Faki Mahamat, pia alisisitiza haja ya dharura ya kushughulikia suala la Palestina.