Rais wa China atuma salamu za pongezi kwa Mkutano wa 37 wa Umoja wa Afrika
2024-02-19 10:26:32| CRI
Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa kufunguliwa kwa Mkutano wa 37 wa Kilele wa Umoja wa Afrika.
Rais Xi amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayakutokea katika karne moja, na maendeleo ya kasi ya "Dunia ya Kusini" inayowakilishwa na China na Afrika inaathiri mchakato wa historia ya dunia.
Amesisitiza kuwa, katika mwaka uliopita, uhusiano kati ya China na Afrika umeendelea kukua kwa kina, na mazungumzo ya viongozi wa China na Afrika yalifanyika kwa mafanikio, ambapo pande hizo mbili ziliamua kuungana mkono katika kutafuta njia zao za kutumia mambo ya kisasa, na kuanzisha mazingira mazuri ya kutimiza malengo yao ya maendeleo. Ameongeza kuwa mwaka huu mkutano mpya wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika, anapenda kushirikiana na viongozi wa nchi za Afrika kutunga kwa makini mpango mpya wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili, unaolenga kunufaisha watu, na kuhimiza ujenzi wa kiwango cha juu wa jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja.