Tume ya kulinda amani ya UM yatuma walinzi wa amani ili kulinda miji miwili muhimu huko mashariki mwa DRC
2024-02-20 09:09:07| CRI

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric Jumatatu alisema, walinzi wa amani wa UM huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanapangwa tena ili kusaidia kulinda miji ya Goma na Sake.

Dujarric alisema kikosi cha kulinda amani cha tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) kinafuatilia kuongezeka kwa hali mbaya zaidi ya mapambano mkoani Kivu Kaskazini.

Alibainisha kuwa kutokana na hali mbaya zaidi ya kiusalama katika maeneo ya Sake na Goma, MONUSCO itaongeza uwepo wake kwa kutuma walinzi wa amani kutoka kikosi cha usaidizi kilichoko Beni, kaskazini mwa mkoa huo. Amesema walinzi wa amani wamesisitiza tena wito kwa kundi la M23 lisitishe mashambulizi yao na kuheshimu Mpango wa Luanda.