Watanzania waikosoa sanamu ya Nyerere nchini Ethiopia
2024-02-20 22:48:58| cri

Baadhi ya Watanzania mitandaoni wameeleza wasiwasi wao kuwa sanamu mpya ya kumuenzi mwasisi wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere haifanani naye. Sanamu hiyo ilizinduliwa Jumapili nje ya makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.

Mmoja wa wanamtandao wa kijamii wa Tanzania amesema samanu hiyo ni ishara nzuri, lakini haifanani kabbisa na Mwalimu Nyerere alipokuwa mzee au kijana, mwanamtandao mwingine alisema "huyo sio Nyerere wetu".

Mwaka jana, sanamu ya heshima ya Rais wa kwanza wa Zambia Kenneth Kaunda, ilibidi kuondolewa baada ya wiki kadhaa za ukosoaji, huku watu wakisema kwamba haikufanana naye.