Serikali ya Zanzibar yawahakikishia wadau wa utalii mazingira wezeshi
2024-02-20 10:49:38| cri

Serikali ya Zanzibar imesisitiza dhamira yake ya kuboresha mazingira wezeshi ambayo kwa kushirikiana na wadau, serikali inatarajia kukuza zaidi utalii unaochangia asilimia 30 ya mapato ya serikali.

Waziri wa Utalii na Malikale Zanzibar Bw. Mudrik Ramadhan Soraga, alisema kuna nafasi ya kuboresha utendaji wa sekta hiyo.

Bw Soraga amesema hayo kwenye mkutano wenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau binafsi katika sekta ya utalii. Mkutano huo umeandaliwa na Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT) na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Jumuiya ya Utalii Zanzibar, Wawekezaji (Zati), Jumuiya ya Waendeshaji Watalii Zanzibar (Zato) na Jumuiya ya wenye hoteli ya Zanzibar (HAZ).