Xi asisitiza uimarishaji wa dhamana ya ardhi kwa ajili ya maendeleo ya hali ya juu ya maeneo yenye nguvu za ushindani
2024-02-20 09:15:31| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kwamba uwezo wa dhamana ya ardhi unapaswa kuimarishwa ili kuhakikisha maendeleo ya hali ya juu ya mikoa ambayo ina nguvu za ushindani, na uwezo wa usimamizi wa dharura wa msingi unapaswa kuboreshwa zaidi.

Rais Xi aliyasema hayo alipoongoza mkutano wa nne wa kamati ya kuimarisha mageuzi kwa pande zote ya Kamati Kuu ya 20 ya CPC.

Mkutano huo ulipitia na kupitisha miongozo kuhusu mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa ardhi, kuhimiza mabadiliko ya muundo wa uchumi wa kijani  katika sekta za maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China, kuongeza uwezo wa usimamizi wa dharura mashinani, na kuharakisha uundaji wa mifumo ya kimsingi inayounga mkono uvumbuzi wa kina. Pia ilipitia na kupitisha ripoti ya kazi ya kamati ya mwaka 2023 pamoja na kazi kuu muhimu za kamati katika mwaka 2024.