Kenya yaunga mkono diplomasia inayojumuisha jinsia ili kukuza amani na usalama
2024-02-21 09:16:37| CRI

Serikali ya Kenya imedhamiria kushirikisha jinsia zote huku ikiwa na azma ya kuimarisha amani, usalama, na hatua za kukabiliana na msukosuko wa hali ya hewa, afisa mkuu aliambia kongamano katika mji mkuu Nairobi Jumanne.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Kenya ambaye pia ni Waziri wa Masuala ya Kigeni na Wanadiaspora, Musalia Mudavadi, akiongeza kuwa kufikia usawa wa kijinsia katika masuala ya kidiplomasia kutaimarisha jukumu la Kenya katika kushughulikia migogoro ya kikanda, itikadi kali, umaskini na kutengwa.

Kongamano hilo la "Wanawake na Diplomasia" lililoitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, na Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva na Nairobi, liliwaleta pamoja watunga sera wakuu, wanadiplomasia, wasomi na wanafunzi.