CPC yatoa kanuni zilizorekebishwa za ukaguzi wa nidhamu
2024-02-22 09:13:22| CRI

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imetoa kanuni zilizofanyiwa marekebisho kuhusu ukaguzi wa nidhamu wa Chama.

Kwa mujibu wa waraka uliotolewa na Kamati Kuu ya CPC, chini ya msingi wa katiba ya Chama na mafanikio yaliyopatikana katika uvumbuzi wa kinadharia, kivitendo na kitaasisi wa kazi ya ukaguzi katika zama mpya, kanuni zilizorekebishwa zinaboresha zaidi taasisi, taratibu na mfumo wa uwajibikaji wa ukaguzi wa nidhamu.

Waraka huo umefafanua kuwa kanuni hizo zina umuhimu mkubwa katika kushikilia na kuimarisha uongozi wa Kamati Kuu ya CPC juu ya kazi ya ukaguzi wa Chama, pamoja na kuhimiza maendeleo ya hali ya juu ya ukaguzi huo, na kuzitaka kamati na makundi ya Chama katika ngazi zote kuchukulia masuala ya kusoma na kutekeleza kanuni kama kazi muhimu ya kisiasa.