Tanzania imeorodheshwa miongoni mwa nchi zitakazofanya vizuri kiuchumi barani Afrika kwa mwaka 2024
2024-02-22 23:19:04| cri

Ripoti mpya ya ufanisi na makadirio ya kiuchumi (MEO) iliyotolewa na benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) inakadiria kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa asilimia 6.1, ukizitangulia nchi nyingine za Afrika Mashariki isipokuwa Rwanda ambayo uchumi wake utakua kwa asilimia 7.2.

Tanzania pia imeorodheshwa ya tisa kati ya 11 za Afrika ambazo uchumi wake unakadiriwa kufanya vizuri nyuma ya Niger (asilimia 11.2), Senegal (asilimia 8.2), Libya (asilimia 7.9), Rwanda (asilimia 7.2), Côte d'Ivoire (asilimia 6.8), Ethiopia (asilimia 6.7), Benin (asilimia 6.4). ), na Djibouti (asilimia 6.2).

Mkurugenzi wa AfDB Dk Akinwumi Adesina amesema benki hiyo inakadiria kuwa ukuaji wa uchumi wa bara la Afrika kwa mwaka huu utafikia asilimia 3.8, na ukuaji huo utakuwa wa msingi, licha ya matatizo ya usambazaji umeme kutokana na upungufu katika uzalishaji wa umeme bado yataendelea.