Mwakilishi wa Xi kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya hayati rais wa Namibia
2024-02-23 09:34:09| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning alitangaza Alhamisi kuwa Mwakilishi Maalum wa Rais Xi Jinping wa China na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Jiang Zuojun amesafiri kwenda Namibia Februari 22 kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya hayati Rais wa Namibia Hage Geingob huko Windhoek.