Mkuu wa kamisheni ya AU aeleza wasiwasi wake kuhusu mivutano mashariki mwa DR Congo
2024-02-23 09:41:07| CRI

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat ametoa wito wa kupunguzwa kwa mivutano inayoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Faki amesema kuwa uadilifu, usalama, mamlaka na utulivu wa nchi zote katika kanda lazima uhakikishwe, na maisha ya raia yalindwe kabisa. Amesisitiza zaidi kwamba hakutakuwa na suluhu ya kijeshi kwa matatizo na mizozo ndani ya jamii ya Waafrika. Alitoa wito kwa mataifa yote ya kigeni "kujiepusha kabisa kuingilia masuala ya ndani ya nchi zote za Afrika, hasa zile za eneo la Maziwa Makuu.

Mivutano imekuwa ikiongezeka kati ya DRC na nchi jirani ya Rwanda huku kukiwa na mapigano makali mashariki mwa DRC. Umoja wa Mataifa unasema kuwa mivutano hiyo inazidisha matatizo ya rasilimali ambazo tayari ni chache kuwahudumia wakimbizi wa ndani laki 8 katika eneo hilo na milioni 2.5 waliokimbia makazi yao katika jimbo la Kivu Kaskazini lililopo mashariki mwa DRC.