Xi ajibu barua kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Muscatine ya Marekani
2024-02-24 21:19:14| cri

Rais Xi Jinping wa China siku ya Jumamosi ambayo pia ni sikukuu ya taa ya Mwaka wa Dragoni ya Kichina, alijibu barua kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Muscatine iliyopo katika jimbo la Iowa, Marekani ambao walitembelea China mwishoni mwa Januari.

Kwenye barua yake, rais Xi aliwahimiza wanafunzi wa shule hiyo kutembelea tena China na kuwakaribisha vijana zaidi wa Marekani kuja China ili waweze kuiona China halisi, kujenga urafiki halisi na vijana wa China, na kutoa mchango wao katika kuimarisha urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.