CMG yafanya tamasha la sikukuu ya taa la mwaka 2024
2024-02-24 21:22:01| cri

Tarehe 24 Februari, siku ya 15 ya mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo ya China ni sikukuu ya taa, moja ya sikukuu za jadi za China. Tamasha la sikukuu ya taa la mwaka 2024 lililoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG limeonyeshwa kwa sifa ya kipekee ya sikukuu hiyo ya jadi ya taa zenye mapambo kupitia nyimbo za jadi, opera, michezo ya kuigiza, na aina za sanaa nyingine.