Sudan yakanusha madai ya Marekani kwake kuhusu kuzuia ufikiaji wa msaada wa kibinadamu
2024-02-26 09:05:07| criSudan imelaumu taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya kuishutumu serikali ya Sudan kuzuia ufikiaji wa msaada wa kibinadamu kwa waathirika wa mgogoro wa Sudan.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema madai ya Marekani dhidi ya Jeshi la Sudan (SAF) na Serikali ya Sudan kuhusiana na misaada ya kibinadamu na shughuli za kiraia ni "shutuma za uongo”.

Taarifa ya Sudan imesisitiza ahadi ya serikali ya Sudan kwa Azimio la Jeddah kuhusu kuwalinda raia, lililosainiwa tarehe 11 mwezi Mei 2023.