ECOWAS yaziondolea vikwazo Burkina Faso, Mali, Niger
2024-02-26 09:07:16| CRI

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imetangaza kuondoa vikwazo vilivyoweka dhidi ya Burkina Faso, Mali na Niger vilivyokuwa na lengo la kuwashinikiza watawala wa kijeshi katika nchi hizo kurejea katika utaratibu wa kikatiba.

Ofisa mwandamizi wa kamisheni ya ECOWAS Bw. Omar Touray, amesema katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano usio wa kawaida wa jumuiya hiyo uliofanyika mjini Abuja, kuwa vikwazo hivyo vinaondolewa mara moja.

Amesema ECOWAS pia imesema haikupokea ombi lolote kutoka kwa nchi hizo kutaka kujitoa kwenye jumuiya hiyo, na kwamba vikwazo pia vimeondolewa kwa raia wa Mali kuchaguliwa kwenye jumuiya hiyo, na kwa serikali ya Guinea.