AfDB kufadhili mradi wa SGR unaounganisha Tanzania na Burundi, DR Congo
2024-02-26 09:07:55| CRI

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania wamesaini makubaliano ya mkopo wa dola za kimarekani milioni 158.1 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa (SGR), kati ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Makubaliano hayo yamesainiwa kati ya meneja wa AfDB nchini Tanzania Bi. Patricia Laverley na Waziri wa Fedha wa Tanzania Bw. Mwigulu Nchemba mjini Dar es Salaam.

Bw. Nchemba amesema mradi huo una manufaa kwa Tanzania, kwakuwa utaimarisha uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi zisizo na bandari za DRC na Burundi. Bi. Laverley amesema kipaumbele kikuu cha AfDB ni kuziunganisha nchi za Afrika kiuchumi.