Maafisa waandamizi wa CPC wawasilisha ripoti za kazi kwa Xi Jinping na Kamati Kuu ya CPC
2024-02-26 15:46:05| cri

Maafisa waandamizi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) hivi karibuni waliwasilisha ripoti za kazi zao kwa Kamati Kuu ya CPC na katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping.

Baada ya kusoma ripoti zao za kazi, Xi aliwataka kuzingatia kuendeleza China ya kisasa, kutekeleza vyema majukumu yao ya kazi, kuimarisha uwajibikaji wao wa kisiasa, na kujitahidi kwa pamoja kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu na kuendeleza kufufua taifa.