Tamasha la sanaa la Rwanda limeangazia uhai wa utamaduni wa nchi za Afrika
2024-02-26 09:08:40| CRI

Tamasha jipya la sanaa lililozinduliwa na Rwanda limetajwa kutoa jukwaa kwa wasanii na wasimamizi wa mambo ya sanaa wa Afrika kuangalia njia mpya na kujenga mahusiano, huku likiangazia uhai wa tamaduni za kiafrika.

Tamasha hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano na taasisi na idara mbalimbali za Rwanda, ni jukwaa kwa ajili ya Afrika nzima lenye lengo la kuunganisha pamoja fasihi, sanaa za maonyesho, dansi, muziki, sinema, mitindo, sanaa za kidijitali, mambo ya chakula na usanifu.

Tamasha hilo lililokuwa na kauli mbiu ya "sanaa, maarifa na biashara vyakutana," limefanyika kati ya Februari 16 hadi 25 mjini Kigali, ambapo

zaidi ya wasanii 200 kutoka nchi 25 walitumbuiza katika maonyesho 60.