Wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na katibu wa Sekretarieti watoa ripoti za kazi kwa Kamati Kuu ya Chama na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama Xi Jinping
2024-02-27 19:27:08| CRI

Kwa mujibu wa kanuni zinazohusika za Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, katibu wa Sekretarieti, wajumbe wa vikundi vya uongozi vya Chama vya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, pamoja na makatibu wa vikundi vya uongozi vya Chama vya Mahakama Kuu ya Umma na Idara Kuu ya Uendeshaji wa Mashtaka ya Umma zimetoa ripoti ya maandishi kwa Kamati Kuu ya Chama na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama Xi Jinping.

Rais Xi amepitia kwa makini ripoti hizo za kazi na kutoa maagizo muhimu, akisisitiza kuwa inapaswa kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa yenye mtindo wa Kichina, kuimarisha uwajibikaji wa kisiasa, na kufanya juhudi kwa pamoja katika ujenzi wa nchi yenye nguvu kubwa na ustawishaji wa taifa.