Makumi ya watu wauawa baada ya shambulizi msikitini nchini Burkina Faso
2024-02-27 08:41:50| CRI

Shirikisho la Jumuiya za Kiislamu nchini Burkina Faso limesema takriban waumini 14 wa kiislamu wameuawa katika shambulizi dhidi ya msikiti mmoja lililotokea mashariki mwa Burkina Faso.

Waumini hao waliuawa katika shambulizi lililotokea jumapili dhidi ya msikiti huko Natiaboani, katika eneo la Est nchini Burkina Faso.

Watu wenye silaha walishambulia msikiti mmoja huko Natiaboani asubuhi ya jumapili na kuwaua watu hao.

Siku hiyo hiyo, takriban watu 15 waliuawa katika shambulizi dhidi ya kanisa katoliki katika kijiji cha Essakane katika eneo la Sahel kaskazini mwa Burkina Faso, ofisa wa kanisa hilo alisema katika taarifa yake.