Rais wa Sierra Leone kutembelea China
2024-02-27 08:40:47| CRI

Kutokana na mwaliko wa rais Xi Jinping wa China, rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone atafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 27 Februari hadi tarehe 2 Machi. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema ziara hiyo ya rais Bio itaingiza msukumo mpya katika kukuza kwa pande zote uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Bibi Mao ameeleza kuwa China na Sierra Leone ni marafiki wa jadi. Katika nusu karne iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili, pande hizo mbili zimekuwa zikiungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi makuu ya kila upande, na kuwa na ushirikiano mzuri katika mambo ya kimataifa, haswa wakati wa kupambana na magonjwa ya Ebola na COVID-19.