Mauritius yazuia meli ya Norway kutia nanga kutokana na hofu ya kipindupindu
2024-02-27 10:51:41| cri

Mauritius imeinyima meli ya Norway kibali cha kutia nanga katika mji mkuu wa Port Louis kutokana na hofu ya uwezekano wa kuzuka kwa kipindupindu ndani ya meli hiyo.

Takriban watu 15 kwenye meli hiyo ya Norway Dawn wametengwa kwa sababu ya kuhisiwa kuwa na ugonjwa huo. Mamlaka ya Mauritius ilisema uamuzi wa kuzuia meli hiyo "ulitolewa ili kuepusha hatari zozote za kiafya".

Sampuli zilichukuliwa juzi kwa majaribio, huku matokeo yakitarajiwa kujulikana jana. Mwakilishi wa “Norwegian Cruise Line Holdings” alisema abiria walipata dalili kidogo za ugonjwa wa tumbo wakati wa safari ya Afrika Kusini. Abiria wa Uholanzi kwenye meli hiyo alisema waliambiwa na nahodha kwamba kunaweza kuwa na mlipuko wa kipindupindu ndani ya meli.

Katika miezi michache iliyopita kumekuwa na milipuko ya kipindupindu kusini mwa Afrika, huku Zambia ikiwa imeathiri