TRC yazindua majaribio ya kwanza ya treni ya umeme
2024-02-27 10:52:09| cri

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limezindua majaribio yake ya kwanza rasmi ya treni ya kwanza ya umeme nchini humo kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi alisema katika uzinduzi huo kuwa serikali inalenga kuziunganisha nchi jirani kwa reli ya SGR.

Treni hiyo mpya ya kielektroniki inategemewa kubadilisha maisha ya watu na njia ya kufanya biashara ikitoa usafiri wa haraka, salama na wa bei nafuu. Treni hiyo ya 160 km/h itakuwa ya thamani kubwa kwa wasafiri na wafanyabiashara. TRC ilipokea vichwa vitatu vya treni ya umeme na mabehewa 27 mapya kabisa ya abiria mwezi Disemba mwaka jana.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema majaribio ya sehemu ya pili kati ya Morogoro na Makutopora yataanza mwezi ujao.