Maonyesho ya vitu vya kale vya Misri kufanyika mjini Shanghai, China
2024-02-27 10:54:07| cri

Jumba la makumbusho la Shanghai na Kamati kuu ya vitu vya kale ya Misri tarehe 25 Februari 2024 walifanya hafla ya kusaini makubaliano mjini Cairo juu ya Maonyesho ya Ustaarabu wa Kale wa Misri ya 2024.

Maonyesho hayo ya ustaarabu wa Kale wa Msiri yatafanyika kuanzia tarehe 19 Julai 2024 hadi tarehe 17 Agosti mwaka 2025 kwenye Jumba la makumbusho la Shanghai, China. Vitu 787 vya kale vya Misri vitaonyeshwa kwenye maonyesho hayo.