Idadi ya vifo kutokana na ajali ya kupinduka kwa kivuko cha Misri yafikia 10
2024-02-27 08:55:11| criWizara ya Kazi ya Misri ilitoa taarifa tarehe 26 ikisema idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kupinduka kwa kivuko kwenye Bonde la Mto Nile mkoani Giza nchini humo tarehe 25 imeongezeka hadi 10. 

Taarifa hiyo imesema kivuko hicho kilikuwa na watu 15 wakati wa tukio hili, na ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu 10 na majeruhi watano. Wizara ya Kazi ya Misri itatoa msaada wa kijamii kwa familia za marehemu na majeruhi.