Serikali ya Colombia na kundi la waasi wakubali kurejesha mazungumzo ya amani
2024-02-27 10:54:34| cri

Ujumbe wa serikali ya Colombia na kundi la waasi ELN walitoa taarifa ya pamoja tarehe 26 Februari mjini Havana, Cuba, wakisema pande mbili zilimaliza mkutano wa siku tatu, na kukubaliana kuendelea na mazungumzo. Mazungumzo ya amani ya duru ya saba yatafanyika tarehe 8 hadi 22 Aprili huko Venezuela.

Makao makuu ya ELN tarehe 20 Februari yalitoa taarifa yakisema ELN itasimamisha mazungumzo ya amani na serikali kutokana na mpango wa serikali wa kufanya mazungumzo mapya mkoani Narino, ambao hauendani na makubaliano ya amani yaliyofikiwa na pande mbili hapo awali. Ujumbe wa serikali ya Colombia ulisema serikali inapenda kutafuta ufumbuzi, kwani kusimamisha mazungumzo kutasababisha mgogoro usio wa lazima. Chini ya uratibu wa pande mbalimbali, pande hizo mbili zilikutana tarehe 24 mjini Havana, ili kutatua tofauti.